Latest News
Posted On: May 06, 2026
|
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA AFYA MAMLAKA YA DAWA NA VIFAA TIBA |
|
ISO 9001: 2015 IMETHIBITISHWA
TAARIFA KWA WATAALAMU WA MAABARA
04 Mei, 2026
MWALIKO WA KUSHIRIKI KIKAO KUHUSU UDHIBITI WA VIFAA TIBA NA VITENDANISHI
- TMDA kwa kushirikiana na Chama cha Wanasayansi wa Maabara za Afya Tanzania (MeLSAT) inapenda kuwaalika wataalamu wote wa maabara kwenye kikao cha pamoja kujadili udhibiti wa vifaa tiba na vitendanishi. Kikao hiki ni muendelezo wa juhudi za Mamlaka za kuwafikia wadau wake ili kuimarisha udhibiti wa bidhaa hizo kwa nia ya kuendelea kulinda afya ya jamii.
- Kikao kitafanyika kwa njia ya mtandao kwa siku mbili tarehe 13 na 14 Mei, 2026 kwa kuwa na ajenda zifuatazo;
- Taratibu za usajili na utambuzi wa bidhaa nchini;
- Taratibu za ukaguzi wa maabara na maduka ya vifaa tiba na vitendanishi na Mkataba wa makubaliano (MoU) na PHLB;
- Utoaji wa taarifa na jinsi ya kushughulikia bidhaa za vifaa tiba na vitendanishi zisizokubalika na zisizofaa;
- Udhibiti wa matangazo ya vifaa tiba na vitendanishi;
- Uhakiki wa utendaji kazi wa vitendanishi vilivyowasilishwa nchini kwaajili ya kuomba usajili.
- Utaratibu na namna ya kushiriki kikao umeanishwa hapa chini: -
Tarehe ya kikao: 13 na 14 Mei, 2026
Muda wa kikao: Saa 7:40 mchana mpaka saa 10:00 jioni
Kiunganishi cha kikao (link):):(Meeting ID: 882 8747 8510, Passcode: 769666) https://us06web.zoom.us/j/88287478510?pwd=pqsc275bmrqYuXw7G5VJi6RdcRPR9v.1 - Wataalamu wote wa maabara mnaombwa kushiriki kikamilifu katika kikao hiki ili kujadili changamoto zinazojitokeza wakati wa utekelezaji wa majukumu yenu ya kila siku ikiwa ni pamoja na kuweka mikakati thabiti ya kuhakikisha usalama wa afya ya wananchi.
- Tafadhali thibitisha ushiriki wako kwa kutuma barua pepe kupitia: octavian.aron@tmda.go.tz au namba ya simu: 0752349590.
- Tunatanguliza shukrani kwa ushirikiano wako.
Mkurugenzi Mkuu,
Mamlaka ya Dawa na Vifaa tiba (TMDA),
Kitalu Na. 56/1, Block E, Kisasa B Centre, Barabara ya Hombolo, S. L. P 1253, Dodoma au
S. L. P 77150, Dar es Salaam
Simu: +255 22 2452108/2450512/2450751
Nukushi: +255 22 2450793
Simu bila malipo: 0800110084