Latest News
Posted On: Feb 09, 2022
|
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA AFYA MAMLAKA YA DAWA NA VIFAA TIBA |
|
IMETHIBITISHWA KWA: ISO 9001: 2015
TAARIFA KWA UMMA
KUHUISHA TAARIFA ZA MAJENGO YA BIASHARA YALIYOSAJILIWA NA TMDA
- Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) inapenda kuwajulisha wafanyabiashara wote wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi waliosajiliwa na TMDA kuhuisha taarifa za majengo yao pamoja na vibali vya kufanya biashara hadi ifikapo tarehe 30 Juni 2022.
- Ili kufanikisha zoezi hilo, wafanyabiashara wote wanatakiwa kufika katika ofisi za kanda za TMDA na kuwasiliana na Mameneja husika kuanzia saa 3.00 asubuhi hadi saa 8.00 mchana.
- Aidha, kwa wale ambao waliwasilisha maombi ya usajili wa majengo kwa njia ya kielektroniki (online submission) watatakiwa kuingia katika tovuti ya TMDA www.tmda.go.tz na kuchagua E-services kisha bonyeza online premises (https://imis2.tmda.go.tz/portal/#/public/app-home) ili kuingia katika mfumo wa TMDA wa wateja (RIMS customer self service portal) na kuhuisha taarifa zao.
- Tunapenda kuwafahamisha wateja wetu kuwa kushindwa kufanya uhuishaji wa taarifa za majengo yao kutasababisha majengo hayo kufutwa katika orodha ya majengo yaliyosajiliwa na TMDA.
- Hatua ambayo itasababisha pale wanapohitaji kuendelea na biashara, kutakiwa kusajili upya majengo hayo.
Mkurugenzi Mkuu,
Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA),
S.L.P 1253 Dodoma au
S.L.P 77150, Dar es Salaam
Simu: +255 222 450512/450751/452108
Simu ya Bure: 0800110084
Nukushi: +255 222 450793
Barua Pepe: info@tmda.go.tz Tovuti: www.tmda.go.tz