Latest News
Posted On: Apr 17, 2021


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA AFYA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA WAZEE NA WATOTO

MAMLAKA YA DAWA NA VIFAA TIBA




ISO 9001: 2015 IMETHIBITISHWA

TAARIFA KWA UMMA

UWEPO KATIKA SOKO WA DAWA BANDIA YA MIFUGO AINA YA ALBEN BLUE 2.5% TOLEO NA. 019394

  1. TMDA inapenda kuutangazia umma kwamba kupitia mifumo yake ya ukaguzi na ufuatiliaji wa bidhaa katika soko imebaini uwepo katika soko wa dawa bandia ya mifugo aina ya ALBEN BLUE 2.5% toleo Na. 019394 lililotengenezwa mwezi Nov. 2019 na lenye tarehe ya mwisho wa matumizi Oct. 2022.
  2. Dawa husika inaonesha kwenye lebo yake kuwa inatengenezwa na kiwanda cha Nerix Pharma kwa niaba ya Vetagro and Pulper Co. Ltd Nairobi, Kenya.
  3. Toleo hili lilifanyiwa uchunguzi wa kimaabara ambapo matokeo ya uchunguzi yameonesha kuwa toleo hilo halina kiambata hai.
  4. Maelezo ya namna ya kuitambua dawa bandia yameainishwa kwenye Jedwali hapa chini:-


    Na.

    MAELEZO

    DAWA BANDIA

    DAWA HALISI

    1.

    Tarehe ya kutengenezwa

    Nov. 2019

    Nov. 2018

    2.

    Tarehe ya kuisha muda wa matumizi

    Okt. 2022

    Okt. 2020

    3.

    Rangi ya kifuniko

    Bluu bahari

    Bluu iliyokolea

    4.

    Rangi ya lebo yenye picha ya wanyama

    Bluu bahari

    Kijani iliyofifia

    Muonekano wa lebo


    5.

    Muonekano wa lebo (Bandia)

    Muonekano wa lebo (Halisi)



  5. Wafanyabiashara wote waliokutwa na toleo hilo wamefunguliwa mashitaka katika vituo mbali mbali vya Polisi na upelelezi unaendelea ili kuweza kuutambua mtandao mzima unaojihusisha na utengenezaji, usambazaji na uuzaji wa toleo hilo bandia la dawa hii.
  6. Kutokana na kubainika dawa hii, wafugaji wote wanaotumia dawa hii kwa ajili ya kuua minyoo wanaelekezwa kuangalia kwa makini lebo zake na endapo wataona namba za toleo husika watoe taarifa kwenye ofisi za TMDA zilizo karibu au kituo cha polisi.
  7. TMDA inaendelea kuwaomba wananchi wote kuendelea kutoa taarifa ikiwa watabaini kampuni, kikundi, mitandao au mtu yeyote anayejihusisha na utengenezaji, usambazaji au uuzaji wa dawa hii ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa dhidi yao.
Imetolewa na:
Mkurugenzi Mkuu,
Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA),
Jengo la PSSSF, Ghorofa ya 10, Barabara ya Makole,
S. L. P 1253, Dodoma au
S. L. P 77150, Dar es Salaam
Simu: +255 22 2452108/2450512/2450751
Nukushi: +255 22 2450793
Simu bila malipo: 0800110084