Latest News
Posted On: May 16, 2025


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA AFYA

MAMLAKA YA DAWA NA VIFAA TIBA




ISO 9001: 2015 IMETHIBITISHWA

TAARIFA KWA UMMA

15 Mei, 2025

MWALIKO WA KUSHIRIKI KIKAO CHA PAMOJA KWA WATENGENEZAJI NA WABUNIFU WA NDANI WA VIFAA TIBA NA VITENDANISHI

  1. Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) inapenda kuwaalika watengenezaji wote wa vifaa tiba na vitendanishi wa nchini Tanzania pamoja na wabunifu wote wa ndani kushiriki kikao cha pamoja ili kujadili mambo anuai yanayohusiana na sekta hii. Kikao hiki ni muendelezo wa juhudi za Mamlaka za kuwafikia wadau wake ili kuimarisha udhibiti wa bidhaa kwa nia ya kuendelea kulinda afya ya jamii.
  2. Kikao kitafanyika kwa njia ya mtandao na kinategemewa kuwa na ajenda zifuatazo;
    1. Majadiliano ya kina kuhusu taratibu za usajili na utambuzi wa bidhaa nchini hasa kwa watengenezaji wa ndani
    2. Taratibu za ukaguzi wa maeneo ya viwanda na maeneo yanayotengeneza bidhaa hizi
    3. Ufuatiliaji wa usalama wa bidhaa hizi sokoni na wajibu wa watengenezaji katika kuhakikisha uatiliaji huo.
    4. Mengineyo.
  3. Utaratibu wa jinsi ya kushiriki kikao umeanishwa hapa chini; - Tarehe ya kikao: 21/05/2025
    Muda wa kikao: saa 4 asubuhi mpaka saa 7 Mchana
    Kiunganishi cha kikao: https://us06web.zoom.us/j/89145385383? brpwd=abs57jsXQYuzlWiuUXYfweNk3SfXe6.1
  4. Tunapenda kuwahamasisha wadau wote waliotajwa hapo juu kushiriki kikao hiki kikamilifu na bila kukosa ili kuweza kutatua changamoto zinazojitokeza katika shughuli zao lakini pia kuweka mikakati thabiti kuelekea mbele.
  5. Tafadhali thibitisha ushiriki wako kwa kutuma barua pepe: christian.kapinga@tmda.go.tz au namba ya simu: 0714972115.
  6. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Imetolewa Na:
Mkurugenzi Mkuu,
Mamlaka ya Dawa na Vifaa tiba (TMDA),
Kitalu Na. 56/1, Block E, Kisasa B Centre, Barabara ya Hombolo,
S.L.P 1253, Dodoma
Simu: +255 (26) 2961989/2061990/ +255(22) 2450512/2450751/2452108,
Namba ya bure: 0800110084
Barua pepe: info@tmda.go.tz, Tovuti: www.tmda.go.tz