Latest News
Posted On: Dec 10, 2020

MAMLAKA YA DAWA NA VIFAA TIBA

TAARIFA KWA UMMA

UFAFANUZI KUHUSU ULIPAJI WA MALIPO KWA AJILI YA TAFITI ZA WANAFUNZI WA CHUO

  1. Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) pamoja na majukumu iliyopewa kupitia Sheria, ya Dawa na Vifaa Tiba, Sura 219 inadhibiti majaribio ya dawa, vifaa tiba na vitendanishi yanayofanyika hapa nchini.
  2. TMDA inapenda kutoa ufafanuzi kwamba kwa mujibu wa Kanuni za Kudhibiti Majaribio ya Dawa za mwaka 2013 haidhibiti tafiti zinazofanywa na wanafunzi wa vyuo mbalimbali.
  3. Kwa mantiki hii, TMDA haipokei maombi wala ada au tozo yoyote kwenye eneo hili.
  4. Wanafunzi wanatakiwa kupata kibali cha kufanya utafiti kutoka Taaisisi ya Taifa ya Tafiti za Afya (National Institute for Medical Research - NIMR) tu nasio TMDA.
  5. Kwa mujibu wa kifungu 5(1) cha Kanuni za Kudhibiti Majaribio ya Dawa 2013, TMDA inatoa vibali vya majaribio ya dawa kwa makundi yafuatayo:
    • 5.1. Dawa ambazo hazijasajiliwa.
    • 5.2. Dawa ambazo zimesajiliwa lakini maombi ya majaribio yameletwa kwa lengo la kubadili matumizi, kuwalenga wagonjwa, kubadili njia ya matumizi na mabadiliko ya dozi.
  6. Ufafanuzi huu unatolewa kwa vile kumekuwa na mkanganyiko kwenye eneo hili na TMDA inawaomba kuuzingatia.
Imetolewa na:
MkurugenziMkuu,
Mamlaka ya Dawa naVifaaTiba,
S.L.P 1253, Dodoma,
Tanzania
Simu Na. +255 22 2450512 / 2450751 / 2452108
Barua pepe: info@tmda.go.tz