Latest News
Posted On: Jun 03, 2022


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA AFYA

MAMLAKA YA DAWA NA VIFAA TIBA




31 June, 2022

TANGAZO LA MNADA WA HADHARA-TMDA

Wananchi wote mnatangaziwa kwamba Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) itauza kwa njia ya mnada wa hadhara vifaa chakavu vikiwemo samani, vifaa vya ofisi na mashine za maabara. Mnada utafanyika siku ya Jumatano tarehe 15 Juni, 2022 kuanzia saa 4 Asubuhi katika ofisi ndogo za Makao Makuu, Mabibo External, Dar es Salaam.

MASHARTI YA MNADA

  1. Kifaa kitanunuliwa kama kilivyo na mahali kilipo.
  2. Mnunuzi atalazimika kulipa asilimia mia moja (100%) ya thamani yote na kuondoa kifaa/vifaa atakavyonunua siku ya mnada.
  3. Mnunuzi atakaye tamka bei ya juu na kushindwa kulipa, hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake kwa mujibu wa sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  4. Ruhusa ya kuangalia vifaa hivyo vinavyotarajiwa kuuzwa itatolewa siku hiyo hiyo ya mnada.
  5. Baada ya kukamilisha malipo vifaa vitaondolewa siku hiyo hiyo ya mnada.
Imetolewa na:
MKURUGENZI MKUU,
MAMLAKA YA DAWA NA VIFAA TIBA,