Latest News
Posted On: Jun 06, 2022


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA AFYA

MAMLAKA YA DAWA NA VIFAA TIBA
IMETHIBITISHWA KWA: ISO 9001: 2015

TAARIFA KWA UMMA

TAARIFA KWA WAFANYABIASHARA WA VIFAA TIBA NA VITENDANISHI KUHUSU MATUMIZI YA AKAUNTI ZA WATEJA WAKATI WA KUOMBA VIBALI KUPITIA MFUMO - ONLINE PORTAL

  1. Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba inapenda kuwataarifu wateja wake wote wa vifaa tiba na vitendanishi kwamba inaendelea na uhakiki wa akaunti za wateja zilizoshikamanishwa na bidhaa zao zilizosajiliwa katika mfumo wa kuomba vibali wa TMDA unaopatikana kupitia anuani imis2.tmda.go.tz/portal.
  2. Katika uhakiki huo imebainika kuwa baadhi ya wateja wamekuwa wakitumia akaunti zaidi ya moja katika mfumo. Hali hiyo inasababisha mteja kushindwa kuziona bidhaa zake alizosajili kwenye mfumo na matokeo yake kuamua kutuma ombi kwa utaratibu maalumu (special import) hivyo kusababisha usumbufu katika kuchakata maombi hayo na hatimaye kuchelewesha utoaji vibali.
  3. TMDA inawataka wateja wenye akaunti zaidi ya moja watoe taarifa ya akaunti ipi iendelee kutumika na ipi ifungwe kabla ya tarehe 30 Juni 2022. Taarifa hiyo itumwe kupitia barua pepe medicaldevices@tmda.go.tz.
  4. Aidha, Mamlaka inapenda kusisitiza kwa wateja wake wote wa vifaa tiba na vitendanishi kusajili bidhaa zao kabla ya kuingizwa nchini ili kuweza kujiridhisha ubora, usalama na ufanisi wake.
  5. Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana nasi kupitia namba ya kupiga bure 0800110084 na baruya pepe info@tmda.go.tz
Imetolewa na:
Mkurugenzi Mkuu
Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba
S.L.P. 1253 Dodoma au 77150 Dar es salaam
Simu +255 22 24521108/2450512/245071
simu ya bure: 0800110084