Latest News
Posted On: Mar 25, 2020

MAMLAKA YA DAWA NA VIFAA TIBA

TAARIFA KWA UMMA

24 Machi 2020

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU HUDUMA ZITOLEWAZO NA MAMLAKA YA DAWA NA VIFAA TIBA WAKATI WA TISHIO LA UGONJWA WA COVID-19

 1. Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) inapenda kuwatangazia wadau wake kwamba kutokana na tishio la ugonjwa wa homa kali ya mapafu ujulikanao kwa jina la Covid-19 ambao unasababishwa na virusi vya Corona, hatua mbalimbali zinaendelea kuchukuliwa na Serikali pamoja na Taasisi zake kama tahadhari dhidi ya maambukizi ya virusi vya ugonjwa huu ambao umeingia nchini.
 2. Hivyo kuanzia tarehe 25 Machi, 2020 huduma za TMDA zitatolewa kwa utaratibu ufuatao:
  1. Vibali vya uingizaji na utoaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vitatolewa kwa kupitia mfumo wa kielektroniki na kutumwa kwa waombaji moja kwa moja.
  2. Maombi ya usajili wa bidhaa yawasilishwe kwa mfumo wa kielektroniki na ufuatiliaji wake ufanywe kwa mawasiliano ya simu na barua pepe kupitia kwa Mameneja wa sehemu husika.
  3. Kwa huduma nyingine ambazo hazitolewi kwa mifumo ya kielektroniki, wateja wanaombwa wafike katika ofisi za TMDA katika maeneo mbalimbali ya nchi endapo tu kuna ulazima huo na wanashauriwa watumie zaidi mawasiliano ya simu na mitandao kupata huduma kupitia maofisa wafuatao:
   Na. Jina la Afisa Cheo Na. ya simu Barua pepe
   1. Bw. Emmanuel Alphonce Meneja, Ukaguzi na Udhibiti wa Dawa na Bidhaa Nyongeza, Ofisi Ndogo TMDA, Dar es Salaam 0754 284367 emmanuel.nkiligi@tmda.go.tz
   2. Bw. Sunday Kisoma Meneja, Udhibiti wa Vifaa Tiba na Vitendanishi, Ofisi Ndogo TMDA, Dar es Salaam 0713 278977 sunday.kisoma@tmda.go.tz
   3. Bw. Felchism Apolnary Meneja, Usajili wa Dawa, Ofisi Ndogo TMDA, Dar es Salaam 0713 477536 felchism.apolinary@tmda.go.tz
   4. Dr. Alex Nkayamba Kaimu Meneja, Udhibiti na Majaribio ya Dawa, Ofisi Ndogo TMDA, Dar es Salaam 0713 868890 alex.nkayamba@tmda.go.tz
   5. Bi. Sophia Ally Kaimu Meneja, TMDA Kanda ya Ziwa, Mwanza 0652565605 sophia.mziray@tmda.go.tz
   6. Bi. Anita Mshighati Kaimu Meneja, TMDA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Mbeya 0687 239387 anitha.mshighati@tmda.go.tz
   7. Bw. Proches Patrick Kaimu Meneja, TMDA Kanda ya Kaskazini, Arusha 0714 836725 proches.kimario@tmda.go.tz
   8. Dr. Edgar Mahundi Meneja, TMDA Kanda ya Magharibi, Tabora 0654 817849 edgar.mahundi@tmda.go.tz
   9. Bi. Sonia Mkumbwa Kaimu Meneja, TMDA Kanda ya Kati, Dodoma 0715 302440 sonia.mkumbwa@tmda.go.tz
   10. Dr. Engelbert Bilashoboka Meneja, TMDA Kanda ya Kusini, Mtwara 0766 729416 engelbert.mbekenga@tmda.go.tz
   11. Bw. Adonis Bitegeko Meneja, TMDA Kanda ya Mashariki, Dar es Salaam 0655 222662 adonis.bitegeko@tmda.go.tz
   12. Bw. Ambele Mwafula Meneja, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano 0713 305193 ambele.mwafula@tmda.go.tz
   13. Bw. Moses Magoma Meneja, Rasilimali Watu na Utawala 0655 888831 moses.magoma@tmda.go.tz
  4. (d) Mamlaka inawaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza katika kipindi hiki cha mpito.
Imetolewa na:
Kaimu Mkurugenzi Mkuu,
Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA),
Mtaa wa Mwanza, Kitalu T, Kiwanja Na.6
S.L.P 1253, Dodoma Au
S.L.P 77150, Dar es Salaam
Simu: +255 22 2452108/2450512/2450751
Simu bila Malipo: 0800110084
Barua Pepe: info@tmda.go.tz