Latest News
Posted On: Mar 28, 2022


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA AFYA

MAMLAKA YA DAWA NA VIFAA TIBA




IMETHIBITISHWA KWA ISO 9001: 2015

TAARIFA KWA UMMA

28th Machi, 2022

MFUMO WA KUTUMA, KUPOKEA NA KUFUATILIA MALALAMIKO, MAPENDEKEZO, UFAFANUZI NA PONGEZI (e-Mrejesho)

  1. Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) inapenda kuwajulisha wateja na wadau wake kuwa imeanza kutumia mfumo wa Serikali ujulikanao kama e-Mrejesho.
  2. Mfumo huu ni maalum kwa ajili ya kuwasilisha malalamiko, mapendekezo, pongezi na kuomba ufafanuzi.
  3. Ili kuhakikisha kuwa lalamiko, pendekezo na pongezi zako zinapokelewa na kufanyiwa kazi ndani ya muda uliowekwa kwa mujibu wa Mkataba wa Huduma kwa Mteja, Wateja na Wadau wetu wote mnaombwa kutumia mfumo huu.
  4. Mfumo huu unapatikana kupitia tovuti (www.emrejesho.gov.go.tz)
  5. Aidha, unaweza pia kuwasilisha malalamiko, mapendekezo, pongezi au kuomba ufafanuzi kwa kupiga simu na kuomba kuonana ana kwa ana na Afisa Malalamiko au kupiga *152*00#, kisha kuchagua Na. 9 kwenye simu janja kwa kutumia programu tumishi(Mobile Apps).
  6. Mamlaka inakushukuru kwa ushirikiano wako.
Imetolewa na:
Mkurugenzi Mkuu,
Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA),
S.L. P 1253 Dodoma au S.L.P 77150, Dar es Salaam
Simu: +255 222 450512/450751/452108
Simu ya Bure: 0800110084
Barua Pepe: info@tmda.go.tz Tovuti: www.tmda.go.tz