Latest News
Posted On: Jul 14, 2022


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA AFYA

MAMLAKA YA DAWA NA VIFAA TIBA




IMETHIBITISHWA KWA: ISO 9001: 2015

TAARIFA KWA UMMA

08 Julai, 2022

TAARIFA KWA WAFANYA BIASHARA WA VIFAA TIBA NA VITENDANISHI JUU YA KUHUISHA USAJILI NA UTAMBUZI WA VIFAA TIBA NA VITENDANISHI

  1. Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba inapenda kuwakumbukusha wadau wake wote kuwa usajili wa Vifaa Tiba na Vitendanishi unadumu kwa miaka mitano (5) na utambuzi kwa miaka mitatu (3) ambapo kuhuishwa baada ya muda huo kuisha kutahitajika.Hii ni sambamba na Kifungu namba 17 cha Kanuni za Udhibiti wa Vifaa Tiba (Tanzania Medicines and Medical Devices (Control of Medical Devices) Regulations, 2015).
  2. Hivyo basi, Mamlaka inatoa wito kwa wafanya biashara wote wa Vifaa Tiba na Vitendanishi kutuma maombi ya kuhuisha usajili na utambuzi wa Vifaa Tiba na Vitendanishi kwa maombi yote yaliyopita muda wake.
  3. Aidha Mamlaka inasisitiza kuwa kutokuhuisha usajili na utambuzi wa Vifaa Tiba na Vitendanishi husika utapelekea kushindwa kuingiza bidhaa hizo nchini.
  4. Kwa maelezo na ufafanuzi zaidi wasiliana nasi kupitia barua pepe medicaldevices@tmda.go.tz.
  5. Tunatarajia ushirikiano wenu katika jambo hili.
Imetolewa na:
Mkurugenzi Mkuu
Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba
S. L. P 1253 Dodoma
Au S. L. P 77150, Dar es Salaam
Simu +255 22 24521108/2450512/245071
Simu ya bure: 0800110084