Latest News
Posted On: Aug 20, 2026


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA AFYA

MAMLAKA YA DAWA NA VIFAA TIBA




ISO 9001: 2015 IMETHIBITISHWA

TAARIFA KWA UMMA

20 Agosti, 2026

KUIDHINISHWA NA KUANZA KUTUMIKA KWA KANUNI ZA MAKUNDI YA DAWA ZA MWAKA 2026 (TS. NA. 150)

  1. Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) inapenda kuwataarifu wateja na wadau wake wote kuwa Kanuni za Makundi ya Dawa za mwaka 2026, zimeidhinishwa na Mhe. Waziri wa Afya na kutangazwa katika Gazeti la Serikali kupitia Tangazo la Serikali Namba 150 la tarehe 19 Juni 2026.
  2. Kanuni hizi ambazo zimeandaliwa kwa mujibu wa kifungu 122 (W) cha Sheria ya Dawa na Vifaa Tiba, Sura 219, Toleo lililorekebishwa la mwaka 2023, zimefanya mapitio ya makundi ya dawa za binadamu na mifugo.
  3. Makundi yaliyorejewa yameweka msingi wa kuhifadhi na kugawa dawa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ikiwa ni pamoja na hospitali, famasi binafsi na maduka ya dawa muhimu (DLDM).
  4. Kufuatia kuidhinishwa kwa Kanuni hizi, madaktari, wafamasia na wale wote wanaoandika na kutoa dawa, wanapaswa kupitia Kanuni hizi ili kuweza kufahamu taratibu mpya zilizowekwa.
  5. Kanuni hizi mpya zitadumisha matumizi sahihi ya dawa hapa nchini kwenye sekta zote za dawa za binadamu na mifugo na hivyo kusaidia katika kupunguza usugu wa vimelea kwa dawa chini ya Mpango wa Afya Moja (One Health Approach).
  6. Kanuni hizi mpya ambazo zinabadili kanuni zilizokuwa zinatumika hapo awali za mwaka 2015, TS. Na. 63 zinapatikana kwenye tovuti ya TMDA kupitia tmda.go.tz/publications/51..
Issued by:
Director General,
Tanzania Medicines and Medical Devices Authority
P.O. Box 1253, Dodoma.
Tel; +255 222 450512/658 445222/777 700002
Fax: +255 222450793
Email: info@tmda.go.tz
Website: www.tmda.go.tz