Latest News
Posted On: Jan 02, 2026


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA AFYA

MAMLAKA YA DAWA NA VIFAA TIBA




ISO 9001: 2015 IMETHIBITISHWA

TAARIFA KWA WATAALAMU WA MIONZI

23 Disemba, 2025

MWALIKO WA KUSHIRIKI KIKAO KUHUSU UDHIBITI WA VIFAA TIBA NA VITENDANISHI VYENYE ASILI YA MIONZI

  1. TMDA inapenda kuwaalika wataalamu wote wa mionzi kwenye kikao cha pamoja kujadili udhibiti wa vifaa tiba na vitendanishi. Lengo ni kuimarisha udhibiti wa bidhaa zenye asili ya mionzi na kuendelea kulinda afya ya jamii.
  2. Kikao kitafanyika kwa njia ya mtandao siku ya Jumatano tarehe 07 Januari, 2026 kwa kuwa na ajenda zifuatazo;
    1. Taratibu za usajili na utambuzi wa bidhaa nchini;
    2. Taratibu za ukaguzi wa viwanda vinayotengeneza bidhaa hizi;
    3. Udhibiti wa bidhaa za vifaa tiba na vitendanishi zisizokidhi vigezo vya ubora na usalama;
    4. Udhibiti wa uagizaji na uuzaji wa vifaa tiba na vitendanishi nchini;
    5. Wajibu wa wadau katika ufuatiliaji wa ubora na usalama wa bidhaa hizi katika soko;
    6. Uteketezaji wa vifaa tiba vikubwa vyenye mionzi, na
    7. Mengineyo.
  3. Utaratibu na namna ya kushiriki kikao umeanishwa hapa chini: -
    Tarehe ya kikao: 07/01/2026
    Muda wa kikao: Saa 4:00 asubuhi mpaka saa 7:00 mchana
    Kiunganishi cha kikao (link):
    https://us06web.zoom.us/j/88189745244?pwd=xfvrbjqIm8cXAsl9NcDSwaov4APBWV.1
  4. Wataalamu wote wa mionzi mnaombwa kushiriki kikamilifu katika kikao hiki ili kujadili changamoto zinazojitokeza wakati wa utekelezaji wa majukumu yenu ya kila siku ikiwa ni pamoja na kuweka mikakati thabiti ya kuhakikisha usalama wa afya ya wananchi.
  5. Tafadhali thibitisha ushiriki wako kwa kutuma barua pepe kupitia: octavian.aron@tmda.go.tz au namba ya simu: 0752349590.
  6. Tunatanguliza shukrani kwa ushirikiano wako.
Imetolewa Na:
Mkurugenzi Mkuu,
Mamlaka ya Dawa na Vifaa tiba (TMDA),
Kitalu Na. 56/1, Block E, Kisasa B Centre, Barabara ya Hombolo, S. L. P 1253, Dodoma au
S. L. P 77150, Dar es Salaam
Simu: +255 22 2452108/2450512/2450751
Nukushi: +255 22 2450793
Simu bila malipo: 0800110084