Latest News
Posted On: Aug 17, 2026
|
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA AFYA MAMLAKA YA DAWA NA VIFAA TIBA |
|
ISO 9001: 2015 IMETHIBITISHWA
TAARIFA KWA UMMA
11 Agosti, 2026
KUCHAPISHWA KATIKA GAZETI LA SERIKALI NA KUANZA KUTUMIKA KWA KANUNI ZA UDHIBITI WA DAMU NA MAZAO YA DAMU, 2026 (GN. Na.149)
- Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA) inapenda kuujulisha umma, wataalam wa afya, vituo vya huduma za uongezaji damu salama, vituo vya kutolea huduma za afya, watengenezaji, waingizaji, wauzaji nje ya nchi, pamoja na wadau wote husika kwamba Waziri wa Afya ameidhinisha na kuchapisha katika Gazeti la Serikali Kanuni za Udhibiti wa Damu na Mazao ya Damu, 2026 (GN. Na. 149), ambazo zimeanza kutumika rasmi kuanzia tarehe 19 Juni, 2026.
- Kanuni hizi zimeandaliwa kwa mujibu wa Sheria ya Dawa na Vifaa Tiba, Sura 219, kwa lengo la kuweka mfumo madhubuti wa kisheria utakaohakikisha kuwa huduma zote zinazohusiana na damu na mazao yake nchini Tanzania Bara zinazingatia viwango vya ubora, usalama na ufanisi.
- Miongoni mwa masharti muhimu yaliyobainishwa katika Kanuni hizi ni wajibu wa vituo kupata leseni, kuzingatia matakwa ya usalama, pamoja na kufanya ukaguzi wa udhibiti kwa vituo vyote vya damu, vituo vya uchakataji wa damu, vituo vya kukusanya damu na maeneo ya kuhifadhi damu ndani ya Tanzania Bara.
- Aidha, Kanuni hizi zimeweka masharti kuhusu uingizaji na usafirishaji nje ya nchi wa damu, bidhaa za kibaiolojia na dawa zinazotokana na mazao ya damu, sanjari na kuanzishwa kwa mfumo wa ufuatiliaji usalama wa damu (Haemovigilance) kwa ajili ya kufuatilia na kutoa taarifa za matukio na madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na matumizi ya damu na mazao yake.
- Vituo vyote vya ukusanyaji wa damu, taasisi zinazojihusisha na uchakataji wa damu, hospitali, waingizaji wa damu na mazao ya damu, pamoja na taasisi nyingine zinazohusika, vinatakiwa kuzisoma na kuzielewa ikiwa ni pamoja na kufanya mapitio ya mifumo yao ya utendaji kazi ili kuendana na matakwa ya Kanuni hizi.
- Wadau na wananchi wote kwa jumla wanaweza kupakua nakala ya Kanuni hizi kwa kutembelea tovuti ya TMDA: www.tmda.go.tz.
- Aidha, wadau wote wanatakiwa kuijulisha Mamlaka kuhusu uwepo wa vituo au maeneo yao yanayojihusisha na huduma za damu na mazao ya damu ndani ya siku 90 toka tarehe ya tangazo hili.
- Baada ya kupokea taarifa rasmi kutoka kwa wadau, Mamlaka itafanya zoezi la kutambua na kuhakiki vituo hivyo ili kuthibitisha uhalali wake na kutoa maelekezo zaidi kadri itakavyohitajika.
- Kwa maelezo au ufafanuzi zaidi, wadau wote wanashauriwa kutembelea ofisi za TMDA au kuwasiliana na Mamlaka ili kupata mwongozo zaidi kupitia anuani hapa chini.
| NA. | TMDA MAKAO MAKUU | ANUANI | ||
| 1 | TMDA Makao Makuu | S.L.P 1253 Dodoma | ||
| Simu: +255 22 262961989 | ||||
| Barua pepe: info@tmda.go.tz | ||||
| OFISI ZA KANDA ZA TMDA | ||||
| NA. | KANDA | ANUANI | Mikoa inayohudumiwa | |
| 1 | Kanda ya Kati | S.L.P 163 Morogoro, | 1. Dodoma | |
| Simu: 023 261 5491 | 2. Singida | |||
| Barua pepe: info.morogoro@tmda.go.tz | 3. Morogoro | |||
| 4. Iringa | ||||
| 2 | Kanda ya Ziwa Mashariki | S.L.P 543 Ilemela, Mwanza, | 1. Mwanza | |
| Simu: +255 28 2981224/5 | 2. Mara | |||
| Barua pepe: info.mwanza@tmda.go.tz | 3. Simiyu | |||
| 3 | Kanda ya Mashariki | S.L.P 31356 Dar es Salaam, | 1. Dar es Salaam | |
| Simu: +255 737 226328 / | 2. Pwani | |||
| +255 766 368412 / +255 788 470312 | 3. Tanga | |||
| Barua pepe: info.easternzone@tmda.go.tz | ||||
| 4 | Kanda ya Kaskazini | S.L.P 16609 Arusha, | 1. Arusha | |
| Simu: +255 (27) 2970333, | 2. Kilimanjaro | |||
| +255 737 782442 | 3. Manyara | |||
| Barua pepe: info.arusha@tmda.go.tz | ||||
| 5 | Kanda ya Nyanda za Juu Kusini | S.L.P 6171 Mbeya, | 1. Mbeya | |
| Simu: +255 25 250 4425 | 2. Njombe | |||
| Barua pepe: info.mbeya@tmda.go.tz | 3. Rukwa | |||
| 4. Songwe | ||||
| 6 | Kanda ya Kusini | S.L.P 48 Ruvuma, Songea. | 1. Mtwara | |
| Simu: +255 766729416 | 2. Lindi | |||
| Barua pepe: info.ruvuma@tmda.go.tz | 3. Ruvuma | |||
| 7 | Kanda ya Ziwa Magharibi | S.L.P 240 Geita | 1. Shinyanga | |
| Simu ya Mkononi: +255 654 817 849 | 2. Kagera | |||
| Barua pepe: info.geita@tmda.go.tz | 3. Geita | |||
| 8 | Kanda ya Magharibi | S.L.P 520 Tabora | 1. Tabora | |
| Simu: +255 (26) 2606082 | 2. Kigoma | |||
| Barua pepe: info.tabora@tmda.go.tz | 3. Katavi | |||
Director General,
Tanzania Medicines and Medical Devices Authority
P.O. Box 1253, Dodoma.
Tel; +255 222 450512/658 445222/777 700002
Fax: +255 222450793
Email: info@tmda.go.tz
Website: www.tmda.go.tz