Latest News
Posted On: Jun 09, 2025
|
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA AFYA MAMLAKA YA DAWA NA VIFAA TIBA |
|
ISO 9001: 2015 IMETHIBITISHWA
TAARIFA KWA UMMA
29 Mei, 2025
UTAMBUZI WA WABUNIFU NA WAVUMBUZI WA VIFAA TIBA NA VITENDANISHI NCHINI
- Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) pamoja na mambo mengine ina jukumu la kudhibiti shughuli zote zinazohusu watengenezaji wa vifaa tiba na vitendanishi kwa kuzingatia matakwa ya sasa ya mfumo bora wa uzalishaji/udhibiti wa ubora kama ilivyoainishwa katika Kifungu cha 51 (c) cha Sheria ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania, Sura ya 219.
- Katika kuunga mkono juhudi za Serikali kwa kuwasaidia wazalishaji na wafanyabiashara wazawa na kwa kuzingatia umuhimu wa ubunifu na uvumbuzi wa vifaa tiba nchini, TMDA na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) iliandaa na kusaini Mkataba wa mashirikiano (MoU) ambao umelenga kutumika kama sehemu ya nyezo ya kuwasaidia wabunifu na wavumbuzi wa vifaa tiba na vitendanishi kutambuliwa, kuonyesha vipaji vyao, kukuzwa na kuongozwa ili waweze kufikia lengo ikiwemo kufanya majaribio ya bidhaa zao na kisha kuzindua na kuanza kutumika kwa ajili ya matibabu nchini.
- Hivyo basi, tunapenda kuwatangazia wabunifu na wavumbuzi wote wanaojihusisha na vifaa tiba na vitendanshi kuwasilisha taarifa zao TMDA ili waweze kutambuliwa na kuwafikia kirahisi na kuwasaidia kwa karibu katika masuala ya kiudhibiti wa bidhaa hizo na kufanikisha malengo yao ili kulinda afya ya jamii.
- Aidha, taarifa zinazopaswa kuwasilishwa ni pamoja na: -
- Jina kamili,
- Anuani ya makazi,
- Mawasiliano (Barua pepe na namba ya simu),
- Vifaa tiba au vitendanishi alivyobuni.
- Tafadhali kama unahitaji uelewa kuhusu mada tajwa usisite kuwasiliana na Ofisi za TMDA Makao Makuu au Ofisi za Kanda zilizoko Arusha, Dar es Salaam, Geita, Mbeya, Morogoro, Mwanza, Ruvuma na Tabora.
Mkurugenzi Mkuu,
Mamlaka ya Dawa na Vifaa tiba (TMDA),
Kitalu Na. 56/1, Block E, Kisasa B Centre, Barabara ya Hombolo, S. L. P 1253, Dodoma au
S. L. P 77150, Dar es Salaam
Simu: +255 22 2452108/2450512/2450751
Nukushi: +255 22 2450793
Simu bila malipo: 0800110084